Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC watakosa huduma ya baadhi ya wao kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Simba SC itakua mwenyeji wa mchezo huo, utakaochezwa Jumapili (Februari 13), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kuanzia saa kumi jioni.

Wawakilishi hao pekee wa Tanzania kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, watakosa huduma ya wachezaji Cris Mugalu, Kibu Denisi (Majeruhi) na Benard Morisson aliyesimamishwa kwa utovu wa nidhamu.

Naye kiungo kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama ataukosa mchezo huo, kufutia kanuni za usajili za CAF kumbana.

Chama alisajiliwa CAF akiwa na RS Berkane ya Morocco, hivyo usajili wake wa kurejea Simba SC unampa nafasi ya kucheza michuano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Simba SC imepangwa kundi D na RS Berkane ya Morocco, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na US Gendarmerie ya Niger.

Wazee Young Africans walia na waamuzi
The Hague kuamua kesi ya malipizi ya Uganda na DR Congo