Rais wa Heshima na mwekezaji wa Simba SC, Mohammed Dewji ‘Mo’ na jopo lake, wamewawekea mezani wachezaji Shilingi Bilioni Moja ili waitoe AI Ahly kwenye michuano ya Africa Football League.

Katika michuano hiyo iliyozinduliwa Dar es salaam jana Ijumaa (Oktoba 20) ikihusisha mastaa kibao akiwemo Kocha Arsene Wenger, Mo amewaanmbia pia kama wakimfurahisha zaidi kwa kumheshimisha anaweza kupandwa mzuka na kufanya kufuru zaidi.

Simba SC inarudiana na Ahly Jumanne (Oktoba 24) jijini Cairo, Misri ambapo kwa kushiriki michuano hiyo tayari kama klabu wana uhakika wa Sh 2.5 bilioni.

Kwenye kikao na wachezaji jijini Dar es salaam, Mo aliwaambia kwamba endapo wangeshinda mchezo wa jana Ijumaa (Oktoba 20) angetoa Sh 500 Milioni na ile marudiano atafanya hivyo hivyo.

Kauli hiyo iliwapandisha mzuka wachezaji ambao kwa juma zima walikuwa wakisubiri kauli ya tajiri na bodi yake, kwani wao tayari walikuwa wakiendelea na yao mazoezini na kambini.

Simba SC wamepania kufanya makubwa kwenye mechi ya marudiano kwani wanaamini haijaisha mpaka iishe na wanasaka heshima kuendeleza vaibu la jana Ijumaa (Oktoba 20) Kwa Mkapa.

Katika michuano hiyo ya muda mfupi yenye fedha nyingi, ili kutwaa kombe kila timu italazimika kucheza mechi sita za kivumbi na jasho kama kile cha jana Ijumaa.

Bingwa anabeba Sh 10 bilioni, mshindi wa pili Sh75 bilioni na kucheza nusu fainali Sh 4.3 bilioni.

Simba SC yatanguliza makachero Cairo
Bosi Sevilla afichua mipango ya Sergio Ramos