Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) limesema kuwa litawapima wachezaji wa klabu ya Yanga na Simba kabla ya mchezo wa ngao ya jamii unaotarajiwa kupigwa agosti 23 mwaka huu ili kubaini kama kuna baadhi ya wachezaji wa timu hizo huenda wakatumia dawa za kuongeza nguvu michezoni.
Hayo yamesemwa na Afsa Habari wa TFF, Alfred Lucas ambapo ameeleza kuwa, jambo hilo huwa linafanyika kwa timu zote zinazoshiriki ligi ya TFF, hivyo kuendelea kufanya hivyo ni sawa na mwendelezo wa swala hilo.
Msemaji huyo ameongeza kuwa upimaji huo utasimamiwa na TFF na madaktari ambao watafanya zoezi hilo kwa kuchukua vipimo vya mchezaji yoyote watakaye hitaji kutoka kwa kila klabu.