Katika kusherehekea miaka 61 ya Uhuru, Klabu ya Gofu ya Kiwanda cha sukari Kilombero, imeandaa mashindano ya mchezo huo uliowakutanisha washiriki kutoka katika sehemu mbalimbali.
Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Fakihi Fadhili amesema lengo la mashindano hayo ni kuwakutanisha wachezaji wa mchezo huo, kwa lengo la kubadilishana ujuzi katika maswala ya kibishara.
Aidha, mchezaji wa Timu ya Taifa ya Gofu, Vicky Elias amewataka wazazi kuwahamasisha watoto wao kushiriki kwenye mchezo huo, na kwamba kuna uhitaji wa kuwaandaa wachezaji wapya wa mchezo huo Kitaifa.
Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Gofu cha Tanzania (TGU), Dickson Sika amesema amefurahishwa na mashindano hayo, na kufua kuwa mchezo huo ulitumika kipindi cha harakati za kupigania uhuru.
Awali, mchezaji mkongwe wa Gofu Morris Komba huo kutoka Klabu ya Gofu ya Kilombero, amesema mchezo huo ulianzishwa mwaka 2002 na David Haworth, akishirikiana na Gerrie Odendaal, meneja wa kiwanda hicho kwa wakati huo.