Wachezaji  wawili wa kimataifa wa Yanga, raia wa Zimbabwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko, wameonyesha kiwango kizuri na ikiwa hali itaendelea hivyo, basi wanaweza kuwaniwa na Azam FC baada ya wachezaji wa Azam kusema kuwa wanawahitaji kikosini kwao.

Habari za uhakika ni kuwa, mastaa kadhaa wa Azam FC, wamevutiwa na uwezo wa wachezaji hao na kutoa ushauri kuwa kama wakimalizana na Yanga, wanaweza kuwa na faida kubwa Azam.

Azam inaona ugumu kuwawania

Pindi anapokutana nao uwanjani wakiwa na Yanga na yeye akiwa na Azam.

“Katika kikosi cha Yanga, kuna wachezaji wawili tu ambao ndiyo wanaoninyima usingizi kila nikiwafi kiria, nao ni Ngoma na Kamusoko.

“Jamaa wanajua sana, kama ungekuwa ni uamuzi wangu basi ningewasajili lakini uongozi wetu unatakiwa kufanya hilo mapema na mimi nipo tayari kuusaidia kuhakikisha suala hilo linafanikiwa pindi mikataba yao itakapomalizika,” alisema Wawa.

Wachezaji wengine kadhaa ambao hawakupenda majina yao yaandikwe, wakakiri kuwa Wazimbabwe hao wana kiwango kizuri na kama wakitua klabuni hapo, basi watakuwa msaada mkubwa hasa katika michuano ya kimataifa.

Hata hivyo, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, alipoulizwa juu ya mpango huo, alisema hawezi kulizungumzia hilo kwa sababu wachezaji hao bado wana mikataba na Yanga.

Ngoma na Kamusoko hivi sasa ndiyo wachezaji gumzo visiwani hapa kutokana na uwezo wao mkubwa wa kutandaza soka waliouonyesha hivi karibuni katika mechi zote za michuano ya Kombe la Mapinduzi walizocheza mpaka sasa.

Msimamizi wa Bomobomoa aanguka Ghafla Ofisini, Madaktari washindwa Kubaini Tatizo
Ronald Koeman Asimamia Msimamo Wake