Kocha Mkuu wa Young Africans Nesreddine Nabi amesema amekuwa akiwasisitiza wachezaji kujituma na kufuata maelekezo anayowapa kuhakikisha wanafanikia malengo yao.
Amesema baada ya kumaliza michezo 19 na sasa wanatakiwa kuwa makini katika mzunguko wa pili kuhakikisha wanafikia malengo yao ya msimu huu ya kutwaa ubingwa wa ligi na ‘ASFC’.
“Wachezaji wanatakiwa kuwa makini kwa sababu michezo iliyobaki kwa sasa yote ni kama fainali na kila mmoja anatakiwa kutimiza majukumu yake ipasavyo akiwa uwanjani,” amesema Nabi.
Amesema kwa wanaelekeza nguvu zao kwa mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la ‘ASFC’ dhidi ya Geita Gold FC, kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
“Tumemaliza mchezo na Azam FC na sasa tunajiaandaa dhidi ya Geita Gold FC, tunafanyia kazi mapungufu yetu na ubora wa wapinzani wetu kuhakikisha tunapata matokeo mazuri na kucheza Nusu Fainali ya ‘ASFC’.
Young Africans itakuwa nyumbani ikiwakaribisha Geita Gold katika mchezo huo utakaopigwa, Aprili 10 mwaka huu katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.