Wachimbaji 15 wa madini ya dhahabu katika Mgodi wa RD Nyarugusu waliokuwa wamefukiwa na kifusi Mkoani Geita wameokolewa wakiwa hai baada ya serikali na wadau mbalimbali wa uchimbaji madini kushirikiana katika mbinu mbalimbali za kitaalamu.
Wachimbaji hao walifukiwa na kifusi walipokuwa katika shughuli zao za kila siku za kujitaftia kipato ili waweze kuendesha maisha yao ya kila siku.
Aidha Wachimbaji hao wamekaa zaidi ya saa 100 chini ya ardhi na kuzua taharuki kwa ndugu na jamaa zao ambao walikuwa wamekusanyika eneo la mgodi huo wakihofia ndugu zao kupoteza maisha.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani aliungana na uongozi wa mkoa wa Geita kuhakikisha wachimbaji hao wanaokolewa wakiwa hai.
Kalemani aliagiza njia mbadala zitumike ili kuweza kuwafikishia chakuala wachimbaji hao wakati utaratibu mwingine wa uokoaji ukiendela.