Wachimbaji 6 wa madini hawajulikani kama wapo hai ama wamefariki baada ya kufukiwa na maporomoko ya udongo katika mgodi wa Copper Hill Gold Mine uliopo katika eneo la Migori nchini Kenya.
Mwenyekiti wa eneo hilo, Christopher Okello amesema kuwa wachimbaji hao walikuwa katika taratibu za kutoka machimboni wakati ukuta wa udongo ulipoanguka
Waliofukiwa katika machimbo hayo ni pamoja na Ominde Achineg (48), Ochieng Mwalimu (37), Atineo Abongo (26) Odhiambo Opiyo (28), Isiah Otwera (27) na Pascal Ochieng (30).
Aidha, taratibu za kuwaokoa zinaendelea lakini kutokana na ugumu wa miamba waokoaji wanapata ugumu kufanya haraka na hivyo kuagiza gari la uchimbaji miamba kwenda kusaidia
Hata hivyo, haijafahamika mara moja sababu za ukuta huo kuanguka ingawa, Okello amesema kuwa inaweza kuwa imesababishwa na mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo.
-
Kenya yaiva kisayansi kurusha satelaiti yake ya kwanza Japan
-
Ethiopia na Kenya zaunda mkakati wa kupambana na ugaidi
-
Burundi yatakiwa kuruhusu matangazo ya Redio