Ujumbe wa Wachimbaji wadogo wazawa wa Madini wapatao 100 kutoka Nchini Tanzania, umewasili Nchini China kwa ziara ya siku sita yenye lengo la kujifunza Teknolojia ya Uchimbaji.

Wachimbaji hao ambao ni sehemu ya Shirikisho wa Wachimba Madini wadogo Tanzania – FEMATA, pia watatumia nafasi hiyo
kujipatia uzoefu, kutafuta Wawekezaji na kufungua fursa za Kibiashara katika sekta ya Madini.

Msafara huo, uliioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa  Wizara  ya Madini, Msafiri Mbibo pamoja na Rais wa FEMATA umepokelewa Jijini Guangzhou na Konseli Mkuu, Khatib Makenga kwa niaba ya Balozi wa Tanzania Nchini China, Mbelwa Kairuki.

Balozi Mbelwa ni sehemu ya waratibu wa ukamilishaji wa fursa hiyo kwa Wachimba Madini waliotembelea maeneo mbalimbali China, inayounganisha Wawekezaji wa Nchi hiyo na Tanzania.

Mikakati ya ECOWAS: Jeshi lamtishia kifo Rais
Dkt. Kikwete ahimiza amani nchi za SADC