Wizara ya haki ya Marekani imesema raia wawili wa China wamefunguliwa mashtaka kwa kujaribu kuiba utafiti wa chanjo ya virusi vya corona na kudukua data za mamia ya makampuni Marekani na nje ya Marekani.

Kulingana na naibu mwanasheria mkuu, John Demers, Li Xiaoyu mwenye umri wa miaka 34 na Dong Jiazhi mwenye miaka 33 pia waliwalenga wanaharakati wa haki za binadamu Marekani, China na Hong Kong.

Wizara hiyo inasema Li na Dong ambao walisomea uhandisi wa mitambo pamoja wamekuwa wakihusika katika masuala ya udukuzi wa kompyuta katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita.

Inadaiwa walikuwa wanazilenga kampuni za teknolojia huko California, Massachusets, Maryland na kwengineko ila hawakuonekana kutatiza utafiti wowote kuhusiana na chanjo ya virusi vya corona.

Haya yanajiri wakati ambapo mahusiano baina ya China na Marekani yakiwa yamevurugika.

Diamond akabidhi kompyuta kwa watoto yatima
Hitimana: Bigirimana atawavaa Simba SC