Chama cha soka Mkoa wa Dar es Salaam, DRFA kwa kushirikiana na Kampuni ya mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, taifa stars na vilabu vya Simba na Yanga na mchezaji Ivo Mapunda, wameandaa majaribio kwa wachezaji wa jinsia zote.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, katika hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu vya soka, Mapunda amesema wachezaji wanaotakiwa ni kuanzia umri wa miaka 6 hadi 20.

Katika kuthibitisha mpango huo, golikipa maarufu Ivo Mapunda ametoa msaada wa vitabu miatano kwa mtunzi wa kitabu cha Soka kinachoitwa Boresha na Endeleza Kipaji chako cha Soka, Juma Gambolii.

Kwa mujibu  wa waandaaji hao, watakaovutiwa na mpango huo wanatakiwa kuchukua fomu na vitabu katika maeneo ya Kimara Mwisho sehemu ya kuuza magazeti, Tabata Shule, Banana, Magomeni Kanisania, Mwenge kituo cha mabasi, mbagara Zakhem kituo cha basi pamoja na mawakala watakaopita mitaani.

Lwandamina achekelea kurudi kwa Tshishimbi
Urusi yafungiwa kushiriki Olympiki