Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuhimizana na kusambaza elimu kwa wale wanaokataa kutoa michango ya chakula shuleni.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa Kagera, Albert Chalamila hivi karibuni Mkoani Kagera na kuongeza kuwa wengi wa wanaokataa kutoa mchango huo hawana sababu za msingi.
Amesema, “wapo wazazi wamewapeleka watoto wao kwenye shule za kawaida na pengine bure kabisa ila ukimwambia mchango wa uji na chakula kwa mtoto wake maelezo yanakuwa mengi, sasa nendeni mkawe mabalozi wazuri huko.”