Viongozi vya vyama vya upinzani waliowahi kujiapisha Barani Afrika inazidi kuongezeka mara baada ya jana kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga kujiapisha.
Odinga siyo mtu wa kwanza kufanya kitu kama hicho, kwani kiongozi wa chama cha upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye alifanya hivyo baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.
Aidha, Etienne Tshisekedi alikuwa kiongozi mkuu wa upinzani, wakati wa utawala wa Rais Mobutu Sese Seko wa Zaire, DRC, na baadaye Laurent Kabila.
November 2011 Tshisekedi aliposhindwa katika uchaguzi dhidi ya mtoto wa Laurent Kabila, Joseph Kabila ambaye ndiye rais wa sasa aliamua kujiandalia kiapo mwenyewe na kuapishwa nyumbani kwake na mkuu wa watumishi wake Albert Moleka baada ya jaribio la kujiapisha katika uwanja wa Wahanga Kinshasa kutibuka.
-
Chama cha SPD chataka kuanza upya mazungumzo na CDU na CSU
-
Obasanjo amtaka Buhari kupumzika masuala ya siasa