Waziri wa Mambo ya na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax amekutana na kuzungumza na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria jijini Vienna kwa ajili ya kuwashawishi wafanyabiashara hao waje nchini kuwekeza, kufanya biashara na kutembelea vivutio vya utalii.

Dkt. Tax ameshiriki kikao hicho pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Bodi ya Utalii Tanzania – TTB, ambapo kwa pamoja walielezea jinsi serikali ilivyoboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji nchini, waliwashawishi kwamba Tanzania ni salama.

Katika kikao hicho, Wamewaelezea Wafanyabiashara wa Austria juu ya faida zinazoweza kupatikana kupitia uwekezaji au ubia na Serikali ya Tanzania au mtu binafsi na kuwahakikishia kuwa Tanzania ni nchi yenye amani na usalama, hivyo ni kituo muafaka kwao kuwekeza na kufanya biashara.

“Tanzania ni nchi yenye amani na usalama, kiufupi Tanzania ni njema na kwa hivyo mtakuwa na uhakika wa kurejesha fedha zenu mlizoweka kwa kuwa na soko la uhakika na faida pia mtapata kutokana na usalama wa mitaji yenu na kufanya biashara,” alisema Waziri Tax.

Akizungumza katika mkutano huo Mwakilishi wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar – ZIPA, Khamis Dunia alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefungua milango ya uwekezaji na kuwakaribisha wenye nia ya kuwekeza Zanzibar katika maeneo ya utalii na miundombinu waje nchini kuwekeza na kujionea vivutio.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania – TIC, amesema Serikali imeunganisha mifumo ya taasisi za usajili na uwezeshaji biashara ili kutoa huduma bora kwa wawekezaji. Taasisi hizo zinajumuisha TIC, NIDA, TRA, BRELA, Uhamiaji na Idara ya Kazi.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania – TTB, Damas Mfugale kwa upande wake aliwambia wafanyabiashara hao kuwa, eneo upo wa aina nyingi ambazo wawekezaji wanaweza kuja nchini na kutembelea maeneo hayo na kuwekeza.

Nyaraka za siri USA: Trump akana mashitaka
Siku ya mtoto Afrika: TAMWA ZNZ waandaa kongamano