Wafanyabishara wa soko, wauza mitumba (WARUMBA) na watumiaji wa Stendi eneo la Mtongani Mlandizi, wilayani Kibaha wamezuia msafara wa Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo kupinga kuhamia kwenye eneo jipya la Mama Salmini ambako wanadai hakuna maslahi kwao.
Kufuatia hali hiyo Waziri Jafo ametoa maelekezo kuwa kutokana na soko hilo kutokuwa mali ya Serikali ni ya mtu binafsi kwa maslahi mapana ya wananchi, wanaotaka kutumia soko hilo la mama salmini wawe huru na wale wanaotegemea Mlandizi waendelee huku wakisubiri ukamilishaji wa soko jipya.
Kuhusu stendi, Jafo amesema medereva daladala wanapata shida na stendi wawe na uhuru, chini ya usimamizi wa wilaya waendelee kutumia stendi ya mlandizi hadi hapo stendi itakapokmilika.
Akizingumza na wafanyabiashara hao, alieleza wafanyabiashara hao waachiwe wafenye biashara kwa utaratibu na kufuata sheria bila kubughudhiwa.
“Nimeangalia idadi ya watu na eneo hilo la mama Salmini wenye hiari ya kufanya biashara wafanye biashara kwenye eneo hilo,lakini na wanaotegemea biashara Mlandizi waendelee “alisisitiza Jafo.
“Mnajengewa soko la kisasa na serikali ipo kwenye mchakato wa kujengwa stendi mpya,hivyo taratibu nyingine zitafuata.”
Hata hivyo, Jafo alifafanua, Watu wadogo wasinyanyasike ofisi ya mkuu wa wilaya na halmashauri iangalie utaratibu wa kuwasogeza kwenye eneo lisilo hatarishi na wafanya biashara wafuate utaratibu, sheria na utaratibu hadi hapo soko maalum litakapokamilika.
“Wafanyabiashara toeni ushirikiano na serikali ya chama cha mapinduzi kwa maslahi ya wilaya na mkoa. “alisema Jafo.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa,aliwataka wawe watulivu na kutoa ushirikiano kwa serikali. Kwa upande wake mwenyekiti wa Warumba ,Nasoro Soma alisema kuwa wao hawako tayari kwenda kufanyabiashara kwenye soko jipya kutokana na mazingira yake hayako vizuri kibiashara.