Wafanyabiashara Nchini wametakiwa kuwa wabobezi katika ajenda ya ulipaji kodi kwa kutumia Mashine za Risiti za Kielektroniki (EFD), kwa lengo la kutunza kumbukumbu za mauzo.

Akizungumza hii leo Desemba 5, 2023 katika maadhimisho ya siku ya mlipa kodi yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Jijini Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri amesema kutokulipa kodi ni ni sawa na kujidhulumu.

“Leo ni siku ya kipekee na ya shukurani kwa walipakodi wa Dodoma kwa kutambua mchango wa wafanyabiashara walioutoa kwa serikali na Mkoa katika mwaka wa fedha 2022/2023,” amesema.

Hata hivyo amewaomba Wafanya biashara hao kuwahamasisha wengine ambao hawazitumii mashine hizo za risiti za kieletroniki.

“Na nyie ndio Mtakuwa waamasishaji wakubwa katika hili , tumategemea kuona wingi wa wafanya biashara wanaamasika katika kutumia mashine hizi za kielektroniki“. Amesema Shekimweri

Shekimweri amesema kuwa hivi karibuni walikuwa na Baraza la Biashara mkoani hapo moja ya hoja zilozungumzwa ni kuanguka kwa biashara ambazo zinafanywa kienyeji kwa kukwepa kulipa kodi.

“Kama mtu unakwepa kulipa kodi huwezi kuzipata fursa za kukopeshwa kwa kuwa unakwepa kodi, kiuhalisia unatakiwa ukopeshwe milioni 100 lakini huwezi kupata ndio maana unakuta mtu anabaishara hiyo hiyo miaka 10 hawezi kubadilika,” amesema.

Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Castro John amewataka wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati ambapo mwezi Desemba ni wa kulipa kodi awamu ya nne na mpaka ifikapo mwishoni mwa mwezi Wafanyabiashara wote wawe wameshalipa kodi husika.

Baleke, Chama, Saido kuongezewa dozi Simba SC
Nahodha SSC Napoli ajitetea kwa kichapo