Wafanyabiashara wa nyama na mifugo jijini Mwanza wamesitisha zoezi la uchinjaji wa ng’ombe kwa siku ya pili sasa kutokana na ongezeko la ushuru wa huduma ya uchinjaji.

Huduma hiyo imedaiwa kupanda kutoka shilingi 2000 hadi 6500 kwa kila ng’ombe huku mnada wa mifugo hiyo ukidaiwa kuhamishwa wilayani Misungwi eneo ambalo ni mbali na machinjio yalipo hali inayowalazimu kutumia gharama kubwa kusafirisha mifugo.

Machinjio hayo yaliyopo katika kata ya Nyakato iliyopo Halmashauri ya jiji la Mwanza yamesitishwa kwa muda usiojulikana huku wafanyabiashara hao wakiomba serikali kuwapunguzia ushuru.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa nyama na mifugo Tanzania Bara TALIMETA Joshua Machage amemlalamikia Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza kutowashirikisha katika maamuzi ya kupandisha ushuru huo.

Machinjio hayo kwa siku huingiza kiasi cha shilingi laki saba hadi nane hivyo mgomo huo wa wafanyabiashara wa nyama hasa ng’ombe uliodumu kwa siku mbili sasa umeikosesha serikali mapato ambayo hukusanywa na Halmashauri ya jiji la Mwanza.

 

Video: Tundu Lissu aibua mengine mapya ya kushtukiza, Rugemarila alipuka mahakamani
Serikali yajibu tuhuma za Tundu Lissu