Wafanyabiashara wa Mifugo nchini, wametakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa
za kununua na kuuza Mifugo, ili kuepusha changamoto ambazo zinaweza kujitokeza hasa za
kununua mifugo ya wizi.
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi, Simon Pasua wakati alipotembelea mnada wa kimataifa wa Pugu pamoja na Machinjio ya Vingunguti Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhakikisha mifugo yote inayouzwa ni halali kuelekea sikukuu ya Pasaka.
Amesema, Wafugaji na Wafanyabiashara wa mifugo wanatakiwa kuhakikisha wanapelekea mifugo yao katika minada ya Serikali ili kudhibiti matukio ya wizi huku akitoa onyo kwa wafanyabiashara wachache ambao wanakwepa kupeleka mifugo maeneo ya minada kuacha mara moja.
Aidha, Kamishna Pasua pia ametoa wito kwa wafanyabiashara hao kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kama kutatokea tukio la wizi wa mifugo huku Mwenyekiti wa wafanyabishara wa Mifugo katika machinjio ya Vingunguti, Joel Meshack akisema kutokana na elimu na maelekezo waliyoyapata changamoto
mbalimbali zilizokuwa zinawakabili zinaenda kutatuliwa.