Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Theopista Mallya amewataka Wafanyabiashara na Wakulima wakubwa kuweka Kamera za ulinzi kwenye maeneo yao, badala ya kuajili Walinzi wasiokuwa na ujuzi na weledi wa mafunzo au walio zezeeka.

Kamanda Mallya amesema hayo wakati wa hafla ya ugawaji vyeti iliyofanyika Tunduma Wilayani Momba, kwa baadhi ya raia ambao wanamiliki silaha hizo kihalali.

Amesema, katika suala la ulinzi wa mali mbali na kufunga Kamera maalum pia ni vyema kuangalia walinzi waliopatiwa mafunzo, wenye afya njema na weledi katika kutimiza majukumu hayo.

Kamanda Mallya pi amewaagiza Wakuu wa Polisi wa Wilaya kuendesha mafunzo maalum ya ulengaji wa shabaha kwa wamiliki hao wa silaha za kiraia yatakayowakumbusha matumizi sahihi ya silaha hizo na kutokuzitumia kinyume na kanuni, sheria na taratibu za umiliki wa silaha za kiraia.

Zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo?, lilifanyika baada ya wamiliki hao wa silaha za kiraia kupewa mafunzo ya wiki moja yaliyofunguliwa Agosti 7, 2023 na kuhitimishwa rasmi Agosti 12, 2023.

Upendo wa Jeshi la Polisi wafika Gereza kuu Ukonga
Tanzania mwenyeji Mkutano kutokomeza ukeketaji