Kufunguliwa kwa mipaka, uwepo wa mvua za kutosha na muingiliano wa bidhaa katika masoko huru Afrika ya Mashariki kumewaweka Wafanyabiashara katika wakati mgumu kutokana na ushindani uliopo kibiashara kiasi cha kushindwa kumudu gharama za uendeshaji ikichangiwa na maradhi ya Uviko-19 na vita vya Ukrainel..

Hayo, yamebainishwa na baadhi ya wananchi wakiwemo wafanyabiashara, ambao walihojiwa na Dar24 hii leo Oktoba 17, 2022 kuhusu hali halisi ya upandaji wa bei za bidhaa kwa maeneo mengi nchini na kwingineko barani Afrika, huku wakidai ufunguaji wa mipaka kiholela kunachangia watu kujipangia bei kulingana na maeneo wanayofanya biashara zao.

Ally Ramadhan, mmojwa waliohojiwa na Dar24 anasema, “Kwa kweli mfumuko wa bei unatuumiza maharage hayashikiki, mchele ndiyo usiseme hali ni tete nadhani ipo haja ya viongozi wetu kukaa chini maana wao sidhani kama hili linawakuta wao wanaendesha maisha yao kwa kodi za wananchi sasa maumivu ya huku ni ngumu kuyafahamu wazungumze na sisi tuwape ukweli wasinyamaze tunaumia.”

Ameongeza kuwa, “Kilo ya maharage mfano kwasasa 3,800 na huyo anayenunua inategemea anayapeleka wapi kama anaenda kula imeisha hiyo lakini kama anaenda kuuza ina maana naye anaenda kuuza hadi shilingi 4,000 mana naye anataka faida na mlaji wa mwisho ndiyo lazima aumie tutafanyaje sasa.”

Hali ya bei kama inavyoonekana kwenye vibao Soko la Mwananyamala jijini Dar es Salaam hii leo Oktoba 17, 2022.

Kwa upande wake, Greyson Kanola amesema “Hali ni tofauti kwasasa na zipo kaya ambazo zinaendesha maisha yao kwa mlo mmoja maana hawawezi sasa, mkulima anauza kulingana na bei elekezi ya Serikali wale wanaonunua wakiyasafirisha nao wakifikisha mjini wanapandisha bei wanakuja wachuuzi nao wanayachukua jumlajumla sokoni wanaenda nao kupandisha bei niambie hapo inakuwaje?.”

Hassan Madika, maarufu kwa jina la ‘Sharp’ ni mmoja kati ya wafanyabiashara wa vyakula jamii ya nafaka, akihojiwa na kituo hiki amesema, kwa sasa mchele daraja la chini kilo moja ni sh. 2,200 na kwamba bidha hiyo kwa daraja la kwanza kilo imefikia sh. 2,800 – 300 kulingana na maeneo na kuishauri Serikali kuangalia upya hali halisi ya kumpa nafuu mwananchi wa kawaida kwani hali si shwari.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Octoba 18, 2022     
Mo Dewji: Tutafanya mabadiliko, hakuna kurudi nyuma