Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha, amewasomea mashtaka matatu raia  14 wa India ambao ni wanafanya kazi wa Quality Group iliyo chini ya Yusuf Manji leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hati ya mashtaka, iliyosomwa na mwendesha Mashtaka, wa uhamiaji Method Kagoma imewataja washtakiwa hao kuwa ni Rojat Surkar, Jagadish Mamidu, Niladri Maiti, Sivarar Raja Sekaran, Mohammed Taher Shaikh, Bijenda Kumar, Prasoon Kumar Mallik na Nipun Dinbandhu Bhatt.

Wengine ni Pintu Kumar, Anuj Agurwa, Varun Boloor, Arun Kumar Kateel, Avinash Chandratiwari na Vikram Sankhala.

Akisoma hati ya mashtaka, Kagoma amedai kuwa, Februari 13, mwaka huu, huko katika ofisi ya Quality Group Ltd iliyopo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao walikutwa wakiwa na viza zilozoghushiwa za kufanyia kazi.

Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa siku na mahali hapo washtakiwa hao wakiwa raia wa India walikutwa wakiishi nchini Tanzania bila ya kuwa na kibali.

Mahakama iliwaamuru washtakiwa hao kuweka dhamana ya milioni tano kila mmoja na kuleta mdhamini mmoja kila mtu atakayeweka  kiasi hicho cha fedha. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 7, mwaka huu.

Mwanamke aliyekatwa mkono kisa ugumba ashika mimba
Lionel Messi Amshawishi Angel Di Maria