Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi ya Mabenki Tanzania (TIOB), Patrick Mususa amelaani kitendo cha wafanyakazi wa benki kutumia simu zao binafsi wakati wa kazi mbadala ametaka zitumike simu za kiofisi ambazo ni simu za mezani kwa mawasiliano.

Amesema kuwa matumizi ya simu binafsi ofisini katika muda wa kazi yanapaswa kudhibitiwa, hii ni kutokana na matukio ya uhalifu yanayotokea mara kwa mara katika kipindi hiki.

Ambapo baadhi ya watendaji wa mabenki  wamehusishwa katika ujambazi na uvamizi wa wateja wanaotoka benki kwa kutumia risasi na kupora fedha.

Hivyo amewataka watumishi wote wanaotumikia benki kutumia simu zao binafsi wakiwa nje ya eneo la benki.

‘’Zitumike simu za ofisi wakati wa kazi tena kwa matumizi ya kiofisi ikiwemo kuwahudumia wateja wao . Mteja anaweza kuruhusiwa kutumia simu yake ndani ya benki pale anapokuwa akifanya miamala na benki husika,’’ amesema Mususa.

Hata hivyo ameeleza kuwa taasisi yake ya TIOB inatoa mafunzo ya kitaaluma na kimaadili jinsi ya ufanyaji kazi katika sekta hiyo.

Na amewataka wamiliki wa Benki kuajili watu ambao wamehitimu mafunzo kupitia TIOB ili wapikwe kimaadili na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

CRDB yamuunga mkono Makonda, yatoa sh. milioni 200
Benedikt Hoewedes kusubiri hadi Oktoba