Huduma za afya katika hospital kuu ya rufaa ya Kenyatta nchini Kenya(KNH),  zimekwama baada ya zaidi ya wafanyakazi 4000 wa sekta ya afya kuanza mgomo wao siku ya Jumatatu kushinikiza nyongeza ya mishahara.

Wafanyakazi wa KNH wanalalamikia hatua ya Tume ya mishahara kutekeleza nyongeza ya mishahara yao ya shilingi milioni 301 iliyopitishwa na bunge na kuidhinishwa na hazina ya kitaifa mwaka 2012.

Katibu Mkuu wa Muungano wa Wauguzi nchini Kenya Seth Panyako, amesema Tume ya SRC imekataa kutekeleza nyongeza mishahara yao licha ya asasi mbalimbaii za serikali kuipatia idhini ya kufanya hivyo.

Mgonjwa mmoja ameripotiwa kufariki huku wengine kadhaa wakiachwa bila njia mbadala ya kupata huduma ya afya.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 29, 2020
Binti anaswa akisafirisha dawa za kulevya