Wafanyakazi wa maduka makubwa ya ‘Uchumi Supermarket’ nchini wamekutana jijini Dar es Salaam kudai stahiki zao wakiwalalamikia wamiliki wa maduka hayo yaliyofungwa.

Wafanyakazi hao ambao wametoka katika maeneo mbalimbali nchini yaliyokuwa na maduka hayo wamewalalamikia wamiliki wa maduka hayo kwa madai kuwa waliwaachisha kazi kinyume cha sheria na baada ya kutangaza kufunga maduka hayo na hawakufanya nao mazungumzo yoyote kuusu hatua zinazofuata.

Kaimu Kamishina msaidizi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Rehema Moyo alikiri kuwa maafisa hao walikiuka taratibu na sheria ya kazi wakati wa mchakato wa kufunga maduka hayo.

“Chini ya hii sheria, mwajiri anaposhindwa kujiendesha, kabla hajawaachisha wafanyakazi inabidi afanye mazungumzo na tawi la chama cha wafanyakazi. Na uchumi supermarket lipo tawi la chama cha wafanyakazi. Kwahiyo alipaswa kufanya consultation wakubaline ili waweze kulipana stahiki zao,” alisema Bi. Moyo.

Uongozi wa Maduka ya Uchumi Supermarket walitangaza kufunga maduka hayo kwa madai kuwa yameshindwa kujiendesha kutokana na kutokuwa na faida bali yanahudumiwa na mapato yanayotokana na maduka hayo yaliyopo nchini Kenya.

Wakata Miwa Waendelea Kujichua Kwa Ligi Kuu
Picha: Lowassa Awatembelea Waliookolewa Mgodini Baada Ya Siku 41, Atoa Mchango Wake