Serikali ya Burundi imeanza kuwakata mishahara watumishi wake ili kuchangia gharama za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya mashirika ya kimataifa kusitisha misaada yao dhidi ya Burundi kugharamia uchaguzi tangu mwaka 2015, baada ya Rais Pierre Nkurunzinza kugombea kuwa rais kwa awamu ya tatu tofauti na katiba ambayo awali iliweka ukomo wa awamu mbili.
Ingawa Serikali ya nchi hiyo inaendelea kufanya mazungumzo na mashirika ya kimataifa kuhusu hatua za kuchangia uchaguzi huo, imeeleza kuwa zoezi la wafanyakazi kuuchangia litakuwa endelevu.
- Chameleone awatimua kwa panga waombolezaji msiba wa Radio
- Dkt Nchemba aeleza Serikali inavyowaneemesha Polisi
“Mazungumzo hayawezi kusimamisha mchakato,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Therence Nthahiraja anakaririwa. “Michango inakuja kutoka kwa mamilioni ya wananchi wa Burundi sio kutoka kwa mtu mmoja au wawili,” aliongeza.
Imeelezwa kuwa kwa wafanyakazi wanaopata mishahara ya kima cha chini wanachangia $2.80 (sawa na shilingi za Tanzania 6,160) kwa mwezi.