Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel na Kituo cha Moyo cha Berlin (Berlin Heart Center) cha nchini Ujerumani wamefanya upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa watoto 15 wenye matatizo ya Moyo.
Upasuaji huo unaotumia mtambo wa Cathlab umefanyika katika kambi maalum ya matibabu iliyoanza tarehe 20/01/2018 inatarajia kumalizika kesho tarehe 25/01/2018.
Aidha, Matibabu yaliyofanyika ni ya kuzibua matundu kwenye moyo na kutanua mishipa ya moyo kwa watoto wenye umri wa kuanzia mwezi mmoja hadi miaka 18.
“Tumepanga kufanya matibabu kwa watoto 20 tunaamini hadi kambi itakapomalizika watoto wote hawa watakuwa wamepata matibabu. Watoto 15 waliopata matibabu wengine wameruhusiwa na waliobaki hali zao zinaendelea vizuri na wataruhusiwa pindi afya zao zitakapoimarika”,”amesema mmoja wa Madaktari
-
Serikali kuendesha mnada wa meno ya Viboko
-
Daktari atoa ripoti ya ukichaa wa ‘nabii Tito’
-
Kandege avunja mkataba wa TBA na Halmashauri
Hata hivyo, Tangu mwaka 2015 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ilianza kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart- SACH) na Berlin Heart Center hadi sasa jumla ya watoto 46 wamefanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel, huku gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa na Taasisi hizi za Israel na Ujerumani kwa makubaliano ya kirafiki na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.