Wafuasi 132 wa Chama cha NUP kinachongozwa na Mwanasiasa wa Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine watafikishwa katika Mahakama ya Kijeshi kujibu mashtaka ya kupatikana na vitu vinavyodaiwa kuwa sare za Jeshi.

Wafuasi hao walikamatwa siku 2 zilizopita wakati Vikosi vya Usalama vilipovamia Makao Makuu ya Chama hicho na kutwaa kofia aina ya Bereti, mavazi mbalimbali na picha za Bobi Wine.

Msemaji wa Polisi eneo la Kampala, Patrick Onyango ameongezea kuwa, vitendo vya vijana kuvalia nembo na mitindo ya Kijeshi imezidi licha ya onyo kutolewa mara kadhaa.

Wanasiasa nchini humo wameeleza kuwa, kesi hiyo ni ya Kisiasa inayolenga kuwatia hofu na mashaka wafuasi wa Bobi Wine katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.


Cedric kitanzini yanga SC.
Serikali yaokoa Shilingi Trilioni 11