Wafugaji wa vijiji vya Kilenzi na Uwemba mkoani Njombe wameulalamikia uongozi wa kiwanda cha maziwa Njombe kwa kukwamisha maendeleo yao.

Wafugaji wa Kijiji cha Kilenzi wamesema kuwa wanakosehwa haki yao kwa kupata malipo yao kwa mda ambao sio muafaka ukilinganisha na muda waliopeleka maziwa katika kiwanda hicho.

“Nina masikitiko kwamba kiwanda kinakokwenda sio kwenyewe kwasababu wakati wapo wale watu weupe, kiwanda kilikuwa kinaenda vizuri sana, lakini kwasasa hivi mambo yamebadilika, yaani badala ya kiwanda kukisimamia vizuri ili kiwasaidie wananchi hilo hakuna,”amesema mmoja wa wafugaji hao. Ditrick Mlyuka

Aidha baadhi ya wafugaji wa kijiji cha Uwemba wameonyesha kusikitishwa na kiwanda hicho kutoa bei mbili tofauti za ununuzi wa maziwa hayo, ambapo kila kijiji kimekuwa na bei yake.

“Tuna masikitiko makubwa sana kwa kuwa utakauta kiwanda kimoja kinatoa bei mbili,kwa mfano kijiji cha Utalingolo wanapewa shilingi mia saba kwa lita, na sisi hapa Uwemba tunapewa shilingi mia tano sitini nayo tunapata sio kwa muda muafaka yaani karibu vipindi vitatu,”wamesema wanakijiji hao.

Kwa upande wake meneja wa kiwanda cha Maziwa Njombe, Edwirn kidehele amekiri kucheleweshwa kwa malipo kwa wafugaji hao.

”Malipo tumeanza kulipa lakini mfumo mzuri wa kulipa vizuri nafikiri mpaka mwishoni mwa mwezi huu wa saba, hiyo mifumo yote itakuwa vizuri, sasa hivi tumeanza kupata oda kubwa kwa hiyo mzunguko wa fedha utakuwa mkubwa,”amesema Kidehele.

 

Video: IGP Sirro atoa kauli polisi kuzuia mikutano ya wapinzani | 'Haponi mtu' CCM
Video: Wakili Manyama ang'ata na kupuliza sakata la Kinana na Makamba