Jeshi la Polisi Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, limewataka Wafugaji kuacha mara moja tabia ya baadhi yao kuingiza mifungo kwenye mashamba ya Wakulima, kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria huku likiwataka kufuga kisasa kulingana na eneo la malisho.

Rai hiyo, imetolewa na Polisi Kata ya Songambele Wilayani humo Makaguzi Msaidizi wa Polisi, Heri Haruba wakati akizungumza na wafugaji katika Mkutano uliofanyika Kijiji cha Orkine Viwanja vya shule shikizi ya Mdung’hu.

Amesema, Jeshi Hilo halitamvumilia mtu anakayevunja Sheria huku akiwataka Wafugaji kufuga kisasa kwa kuwa na mifugo kulingana na maeneo ya malisho, ili kuepuka migogoro na Wakulima hasa kipindi cha kilimo.

Jeshi la Polisi Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, kwa kutumia Polisi Kata limekuwa likitoa elimu ya kubaini, kutanzua na kuzuia uhalifu kwa makundi yote yote katika jamii, ikiwemo wafugaji.

Ajali ya Ndege: Mkuu wa Mkoa atoa ufafanuzi
Waliolipua Kanisa wahukumiwa kunyongwa