Baada ya zoezi la bomoabomoa kulikumba jengo la kanisa la The River of Healing Ministry liliko jijini Dar es Salaam, waumini wa kanisa hilo wamefunga na kuomba porini kuombea zoezi hilo.

Mchungaji wa kanisa hilo, John Kyashama amesema kuwa wameweka kambi katika shamba lake liliko Chalinze kwa siku tatu wakifunga na kuomba wakiamini Mungu atawaonesha sehemu ya kwenda kujenga kanisa lao kabla Serikali haijavunja jengo wanalotumia sasa kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro.

Aidha, Mchungaji huyo alisema kuwa anaheshimu sana uamuzi wa Rais John Magufuli na katika mfungo huo wanamuombea atekeleze majukumu yake kwa haraka zaidi.

“Rais ni taasisi kubwa, naamini Mungu kabla sijavunjiwa kanisa langu atakuwa ameshamfikia na kumpatia eneo jingine, kwa hilo sina shaka, “alisema Mchungaji Kyashama.

Kanisa la The River of Healing Ministry lina waumini takribani 3,000.

Makanisa mengine yaliyipitiwa na zoezi la bomoabomoa ikiwa ni pamoja na kanisa la Rutheran Kibamba yameanza kubomoa yenyewe na kuhamisha huduma katika maeneo mengine.

 

Bill Gate atoa msaada wa mabilioni Tanzania
Video: Roma asimulia alivyotekwa kwenye wimbo mpya 'Zimbabwe'