Daktari Bingwa wa magonjwa ya Saratani Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Crispin Kahesa amewashauri waumini wa kiislamu katika mfungo wa Ramadhani kula chakula chepesi baada ya kufungua (Futuru) kwani humsaidia mfungaji kutopata saratani ya utumbo.
Amesema ”Kufunga ni ibada na ni jambo zuri kwa afya ya binadamu, lakini tunashauri watu kuzingatia kula vyakula vyepesi wakati wa kufungulia na si vile vigumu kwani huweza kuwasababishia matatizo ikiwamo saratani ya utumbo”. Kahesa.
Ameongezea kuwa wapo ambao hufungulia kwa kunywa maji au vyakula vya moto ni sahihi na bora zaidi kuliko wale wanaokula vyakula vigumu.
-
Watu 65 wafariki dunia kwa joto kali
-
Video: Mawaziri wanne, spika na wabunge watifuana, Jina sasa lamponza Makonda
Vyakula vyepesi ni kama vile uji, chai hivyo ndivyo ambavyo tunashauri na vikiwa na moto kidogo ni vizuri kwa sababu vinalifanya tumbo lipate joto na kulishtua kwani linakuwa limekaa muda mrefu bila kupata chakula.
Amesisitiza pia chakula cha Daku kwani husaidia tumbo kutobakia tupu hadi jioni wakati wa kufuturu, amesema kuwa mtu aliyewahi kuugua vidonda vya tumbo yupo hatarani kupata saratani hiyo.