Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa wafungwa 1,631 ikiwamo wa kike walioingia na mimba gerezani wamenufaika na msamaha uliotolewa katika kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Rais Samia, ametoa msamaha huo kwa kuzingatia mamlaka aliyopewa chini ya kifungu 45 (1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo wafungwa wenye sifa stahiki wapunguziwe robo ya adhabu zao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu.

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni imeeleza kuwa chini ya kifungu cha 49 (1) cha sheria ya Magereza sura ya 58 wafungwa hao wawe wamehukumiwa kifungo cha miaka miwili au zaidi ambao wametumikia robo za adhabu zao magerezani.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Na wawe wameingia gerezani kabla ya Septemba 10, mwaka huu isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika sharti la 2, wafungwa wenye magonjwa ya kudumu au sugu ambao wapo hatua za mwisho za ugonjwa na hatua hiyo ithibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa au Mganga mkuu wa Wilaya,” amesema

Ameeleza, katika idadi tajwa wafungwa 101 wataachiliwa huru kuanzia Desemba 10, 2022 na 1530 watabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huo amebainisha kuwa wafungwa wazee wenye umri wa miaka 70 au zaidi ambao wametumikia adhabu zao, umri huo uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa na wa wilaya.

Ameongeza kuwa wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani au wenye watoto wanaonyonya na wasionyonya , wafungwa walemavu wa mwili na akili wasio na uwezo wa kufanya kazi na hali zao zidhibitishwe na jopo la uenyekiti wa Mganga Mkuu wa mkoa na wilaya.

Wafungwa wakiwajibika.

“Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kuwekwa kizuizini ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka 15 au zaidi na wale waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani ambao wametumikia adhabu hiyo kwa miaka 20 au zaidi na waliobadilishiwa adhabu ya kifo na kuwa maisha na wamekaa miaka 20 au zaidi kuanza walipoanza kutumikia adhabu ya kifo,”

Katika hatua nyingine wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa makosa ya kujamiana, utekaji au wizi wa watoto, kuwapa mimba wanafunzi au makosa yanayohusiana na ukatili dhidi ya watoto na biashara haramu ya binadamu ni miongoni mwa makundi ya wafungwa waliokosa msamaha huo.

 “Waliokutwa na nyara za serikali, ujangili na kukutwa na viuongo vya binadamu, makosa ya ubadhilifu wa fedha za umma, wafungwa wa madeni (Civil Prisoners), unyang’anyi wa kutumia nguvu  na ule wa kutumia silaha, risasi, mlipuko au kujaribu kutenda makosa hayo,” amesema

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni.

Pia, msamaha huo haujawahusisha wafungwa waliohukimiwa adhabu ya kunyongwa na wenye makosa ya kujaribu kujiua au kuua watoto wachanga  na wanaotumikia vifungo vya nje chini ya sheria ya Bodi za Paroli sura ya 400(R.E.2002) sheria ya huduma kwa jamii sura 291(R.E. 2002) na kanuni za kifungo cha nje.

“Wengine waliokosa msamaha huo ni waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa mashauriu/ kesi za uhujumu  uchumi na wanaotumikia  kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka ,utakatishaji wa fedha, rushwa, usafirishaji au kujiuhusisha  na  madawa ya kulevya ikiwemo bangi,” amesema Waziri Masauni.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 12, 2022
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 11, 2022