Serikali imepiga marufuku wafungwa kutoka Magereza mbalimbali nchini kutumika katika kazi binafsi isipokuwa kwa kufuata utaratibu unaotambulika kisheria.

Aidha, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Chilo amepiga marufuku mahabusu kurundikwa kwenye vituo vya polisi kisa upelelezi haujakamilika huku akiagiza wapewe dhamana.

Marufuku hiyo imetolewa mkoani Singida na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo wakati wa kikao kilichojumuisha askari polisi kutoka Idara zilizopo chini ya Wizara, ambapo amesema wafungwa wana taratibu zao zinazowaongoza katika mfumo wao mzima wakiwa gerezani huku akiwaagiza Wakuu wa Magereza yote nchini kufuata taratibu hizo.

“Kuna taarifa za uhakika kwa wafungwa kutumika katika shughuli binafsi ikiwemo kujenga nyumba za watu binafsi na kulima mashamba ya watu binafsi, nimpongeze Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee katika kipindi chake ameanza kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha jeshi linarudi katika misingi yake na sasa tunaona magereza inaendelea kuboreka kila uchwao sisi kama serikali tunapiga marufuku matumizi binafsi ya wafungwa katika shughuli yoyote binafsi ila kwa kufuata utaratibu,” amesema Naibu Waziri Khamis Hamza Chilo.

Sambamba na hilo amewataka wakae kwa pamoja kujitathimini na kupiga marufuku kurundika kwa mahabusu badala yake wapewe dhamana kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Mabadiliko Young Africans safi
Samia: Huu sio wakati wa kusikiliza maneno kutoka nje