Waamuzi kutoka nchini Uganda wamepewa jukumu na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ kuchezesha mchezo wa mzunguuko wa tano wa Kombe la Shirikisho Kundi D, kati ya Namungo na Raja Casablanca kutoka nchini Morocco utakaofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, kesho Jumatano (April 21).

‘CAF’ imemtaja mwamuzi Ali Sabila Chelanget ambaye tafanya kazi pamoja na Waganda wenzake, Dick Okello (mwamuzi msaidizi namba moja), Isa Masembe (mwamuzi msaidizi namba mbili) na Mashood Ssali (mwamuzi wa akiba).

Kamishna wa mchezo atakuwa Alemu Gizate kutoka Ethiopia, huku mtathimini waamuzi atakuwa Michel Gasingwa (Rwanda) na mratibu wa jumla ni Kabelo Bosilong (Afrika Kusini).

Ofisa wa covid -19 ni Manfred Limbanga Kinyero  kutoka Tanzania.

Namungo FC wataingia kwenye mchezo huo wa kesho, huku wakifahamu fika hawana nafasi tena ya kusonga mbele kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, baada ya kupoteza michezo minne ya michuano hiyo.

Namungo FC ambao wanashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza, wanaburuza mkia wa msimamo wa Kundi D, wakishindwa kuambulia alama hata moja kwenye michezo yote minne waliyocheza mpaka sasa.

Niyonzima: Asiyetaka Presha aondoke
Waziri wa TAMISEMI amsimamisha kazi Mkurugenzi Sengerema