Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amekiri kuwa walikuwa na baadhi ya wagombea ambao hawakuwa wakikubalika kwenye maeneo waliyogombea nafasi mbalimbali ikiwemo ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Aidha amesema kuwa Chama kuwa na ajenda ya kuwashawishi wananchi kukichangua ambapo, Mbowe amesema CHADEMA haijawahi kukosa ajenda ya kushindana na Chama tawala-CCM.

“Nikiri kuna maeneo mengi tulikuwa na wagombea sahihi, lakini kuna maeneo kadhaa tulikuwa na wagombea dhaifu, huo ni ukweli na haupingiki kwa sababu waswahili wanasema wali wa kushiba unaonekana kwenye sahani,” amesema Mbowe.

Pia, amesema kwa sasa falsafa zake za kisiasa zinakwenda sawa na zile za aliyekuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Marekani, Thomas “Tip” O’Neil Jr.

Amesema O’Neil kupitia kitabu chake cha ‘All Politics is Local’ amesema siri za ushindi za chama cha siasa ambazo ndizo anazutimia kuongoza mapambano ya kushika dola nchini.

Amezitaja falsafa hizo kuwa ni chama kupata mgombea sahihi na nayekubalika kwa wapiga kura.

Aweso: Mradi ukabidhiwe ifikapo Juni 30
Tanzania kuja na kilimo cha Tija