Wagombea wenza wa Urais nchini Kenya, Rigathi Gachagua na Martha Karua wanakabiliana kwa mdahalo wa Naibu rais jijini Nairobi, kushiriki kutoa mitizamo yao huku mada ya ufisadi ikitawala mkutano huo.

“Sina mabilioni,”amesema mgombea mwenza wa William Ruto, huku mgombea mwenza wa Raila Odinga akisisitiza kuwa sheria ni lazima itumike kwa usawa na kwa watu wote.

Gachagua, ni mgombea mwenza wa Naibu Rais William Ruto, huku Karua akichaguliwa na Raila Odinga kuwa Makamu wake wa Urais endapo mmoja kati ya hao atashinda katika uchaguzi mkuu na kuiongoza Kenya.

Rigathi Gachagua.

Hata hivyo, Gachagua alibanwa kwa makosa ya ufisadi mwaka 2021, akiwa msaidizi wa zamani wa Rais Uhuru Kenyatta na alishtakiwa kwa kujipatia zaidi ya Dola 60 milioni katika isivyo halali.

Kwa upande wake Karua. alitetea rekodi yake ya awali kama Waziri, Mwanaharakati, na Mbunge akisema atatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, huku mashambulizi ya kimyakimya kwa Ruto ambaye alitofautiana na Rais Uhuru Kenyatta mwanzoni mwa muhula wao wa pili yakijadiliwa.

Mdahalo mwingine wa wagombea Urais, umepangwa kufanyika Jumanne ijayo, Lakini William Ruto wa Muungano wa Kenya Kwanza ameapa kujiepusha nayo, akivishutumu vyombo vya habari kuwa na upendeleo.

Martha Karua

Wabunge wapiga kura kumchagua Rais mpya
Kemikali yenye sumu yatambuliwa katika miili ya Vijana 21