Jumla ya watu 601 wamefanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo katika kambi maalum ya Madaktari Bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – JKCI, kwa kushirikiana na wale wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa -IRRH.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – JKCI, Pedro Pallagyo amesema katika uchunguzi huo, wametoa rufaa kwa wagonjwa 80 waliohitaji uchunguzi zaidi na kwa wale waliohitaji upasuaji mkubwa na mdogo wa moyo kwenda JKCI, kwa ajili ya kupatiwa matibabu hayo.
Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – JKCI, Gerson Mpondo akimfanyia mgonjwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi.
Amesema wengi waliofanyiwa uchunguzi katika kambi hiyo wamekutwa na magonjwa ya shinikizo la juu la damu, magonjwa ya mishipa ya moyo kuziba na magonjwa ya valvu za moyo kuziba au kuvujisha damu kwenye moyo.
Kambi hiyo ya siku tano pia imetoaji wa mafunzo ya kutumia mashine ya kuchunguza jinsi moyo unavyofanya kazi kwa wataalam wa afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, huku watu wazima 571 na watoto 30 wakipatiwa matibabu ya moyo.