Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema idadi ya watu waliopata maambukizi ya virusi vya Corona nchini yafikia 20, huku wawili wakipona na kuruhusiwa.

Taarifa ya Wizara ya afya nchini Tanzania iliyotolewa leo April mosi imeeleza mgonjwa mpya ni raia wa Marekani ambaye ameingia nchini hivi karibuni na amegundulika akiwa jijini Dar es Salaam.

”Mgonjwa huyo ni raia wa Marekani Mwenye miaka 42 ambaye amekuwa karibu  na mtu aliyesafiri nje ya nchi na baadaye kuthibitika kuwa na maambukizi ya Covid 19 aliporejea nchini”amesema Ummy

Aidha amesema wagonjwa 17 wanaendelea na matibabu na hali zao ni nzuri na jana machi 31 mgonjwa mmoja aliyekuwa kituo cha Temeke aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kuthibitika kupona.

Ambapo hadi sasa Tanzania imekuwa na idadi ya watu wenye maambukizi ya virusi vya Corona 20 huku wawili wakipona na mmoja kufariki dunia.

Ameongeza kuwa Tunasisitiza wananchi kuchukua tahadhari zinazotolewa na wizara ta Afya katika kukabiliana na ugonjwa huo.

 

LIVE Updates: Hali ya Corona Duniani
MOI yapokea viungo bandia vyenye thamani ya Sh 80.9 milioni