Wizara ya Afya nchini Tanzania imethibitisha kuongezeka kwa wagonjwa wengine wapya 29 wa COVID-19 na kufanya hadi sasa Tanzania kufikia idadi ya Wagonjwa 88 .
Wagonjwa hao ni kutoka katika sampuli zilizopimwa tarehe 14 na 15, Aprili 2020 katika maabara ya Taifa na wote wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa wataalam afya.
Ambapo wagonjwa 26 wapo jijini Dar es salaam wawili wapo Mwanza na mmoja yupo Kilimanjaro.