Serikali ya Uganda, imetangaza kugundua visa vipya sita vya Ebola, na hivyo kuongeza idadi ya waliothibitishwa kuugua maradhi hayo kufikia watu saba, huku Gazeti moja la kila siku la nchini humo likiripoti kwa kuzinukuu mamlaka kuwa idadi ya vifo vya Ebola imeongezeka na kufikia watu 12.
Siku ya Jumanne, Septemba 20, 2022 nchi hiyo ya Afrika mashariki ilithibitisha kuzuka kwa homa ya kuvuja damu katika Wilaya ya kati ya Mubende, iliyopo takriban kilomita 150 magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo Kampala na kusema homa hiyo ni aina ya Sudan.
Meneja wa Matukio katika Wizara ya Afya ya Uganda, Kyobe Henry Bbosa amesema, “Habari za janga hilo limeonekana kuanza mwanzoni mwa Septemba baada ya watu kuanza kufa katika kijiji kidogo katika Kaunti Ndogo inayoitwa Madudu.”
Hata hivyo, Siku ya Alhamisi (Septemba 22, 2022), maafisa wa afya wa nchi hiyo walisema watatumia uzoefu wake wa hapo awali ili kukabiliana na milipuko ya hivi karibuni na kuongeza kuwa vituo vya matibabu ya Covid vitageuzwa kuwa vituo vya kudhibiti Ebola.
Kufuatia halihiyo, Kyobe amesema, “Kama tuliweza kulidhibiti kwa mafanikio Covid tunawenga nguvu zaidi katika kuikabili Ebola lakini pia tuna uwezo mkubwa kwa sababu ya vituo vya nje nchini, kwa ajili ya kugundua na pia kuweza kuhimiza usaidizi na mwitikio wa jumuiya.”
Uganda, imekumbwa na milipuko ya awali ya ugonjwa huo hatari ambapo kesi za mwisho zilizoripotiwa zilikuwa za mwaka 2019 kwa kuwa na angalau vifo vitano.