Waziri wa Afya nchini Burundi Thadée Ndikumana ametangaza nchi hiyo kupata Wagonjwa wawili wenye maambukizo ya Covid 19  ambao ni raia wa Burundi wakiwa na miaka 42 na 56

Aidha kati ya wagonjwa hao, mmoja ametokea Rwanda na mwingine Dubai hata hivyo hajatangaza ni lini watu hao waliingia Burundi akidai kuwa kutangaza siku hiyo kutaathiri ufuatiliaji wa watu aliokutana na Wagonjwa

Hata hivyo imesitisha safari zote za ndege za kuingia nakutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Melchior Ndadaye huku nchi za jirani za ikiwemo DRC Congo, Rwanda na Tanzania zikiwa na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona

Katika hatua nyingine  shule za Kifaransa na Ubelgiji nchini humo pamoja na Kituo cha Utamaduni wa Kifaransa zimesimamisha shughuli zake kwa walau siku 15 kutokana na hofu ya Covid 19.

Meddie Kagere afichua usioyajua
Hamdoun apewa programu maalum Azam FC