Hospitali ya Rufaa Nkinga, Tabora kwa kushirikiana na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili – MOI, wamewapatia matibabu ya kibingwa na ya kibobezi Wagonjwa 410, katika kambi maalum ya siku 5, huku wagonjwa 20 wakifanyiwa upasuaji mkubwa.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa Nkinga, Victor Ntundwe ambaye amewashukuru Madaktari bingwa, Wauguzi na Mtaalam wa usingizi wa Taasisi ya MOI kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha katika kambi hiyo iliyowajengea uwezo wataalam.

Amesema, “tumepata shuhuda nyingi kutoka kwa wagonjwa mbalimbali ambao walikuwa hawana uwezo wa kwenda Dar es Salaam kuzifuata huduma hizo na wamefurahi sana kuona huduma hizo zinatolewa hapa hospitali ya Rufaa Nkinga.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface amesema waliweka kambi hiyo kwa lengo la kujengeana uwezo wa kutoa tiba bobezi, ambazo zinapatikana katika Hospitali ya MOI.

Mauaji Wanafunzi 43: Serikali lawamani kutowakamata wahusika
Tuzo za CAF zaipa jeuri Simba SC