Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limewafikisha Mahakamani watuhumiwa wa makosa makubwa ya uhalifu wapatao 106, ambao walipatikana na hatia na kuhukumiwa Jela vifungo mbalimbali ikiwemo watu watano waliohukumiwa vifungo vya miaka 20 kwa makosa ya kupatikana nyara za Serikali..

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP, Justine Masejo amesema watuhumiwa hao walihukumiwa kwa makosa ya Ubakaji, Ulawiti, Kusafirisha dawa za kulevya, unyang’anyi wa kutumia silaha, mauaji na kupatikana na nyara za Serikali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP, Justine Masejo.

Amesema, kati ya wahalifu hao 25 walihukumiwa Vifungo vya maisha jela kwa makosa ya ubakaji, ulawiti na mauaji na watuhumiwa 30 walihukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, kusafirisha dawa za kulevya, ubakaji na ulawiti.

Hata hivyo, Kamanda Masejo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kufichua matukio ya uhalifu katika jamii, ili wachukue hatua za kisheria dhidi ya wote watakaobainikakuwatahadharisha watu wachache wanaojihusisha na matukio ya uhalifu kuacha mara moja.

Yusufu Mhilu aibukia Geita Gold FC
Joao Felix awachefua mashabiki Atletico Madrid