Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, ACP Abdalla Hamis Mussa amewataka wananchi wa Shehia ya Wara Kijiji cha Machomanne Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba kujitokeza na kutoa ushahidi kwa lengo la kukomesha vitendo vya kihalifu hususan Udhalilishaji wa wanawake na watoto.
Kamanda Mussa ameyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita na kuongeza kuwa bila ya Wananchi kujitokeza na kutoa ushahidi, vitendo hivyo haviwezi kumalizika kwani hakuna kesi itakayopata mafanikio, badala yake uhalifu utaendelea.
Kuhusu Udhalilishaji, dawa za kulevya, Wizi, Malezi, mmong’onyoko wa maadili na
Ulinzi shirikishi, amewataka Wananchi pia kushiriki katika kutoa ushahidi baada ya mtuhumiwa kukamatwa, kwani taarifa sahihi zitasaidia kuchukua hatua stahiki.
Jeshi la Polisi Nchini, linaendelea na zoezi lake la uelimishaji Wananchi katika maeneo yote kuanzia ngazi ya Vijiji, Kata, Wilaya na hata Mkoa likilenga kupambana na kuzuia uhalifi kwa kushirikiana na jamii.