Vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Dar es salaam vimewatia mbaroni wahamiaji haramu 36, raia wa Ethiopia na Somalia walioingia nchini kinyume na taratibu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge, amewaonya watanzania wanaoshiriki kuwafadhili na kuwasafirisha kwa ili wapate fedha.

RC Kunenge amesema wahamiaji hao walikamatwa usiku wa kuamkia Novemba 15, kwenye fukwe za Mbweni ambapo kati yao 30 wanatoka nchini Ethiopia na Sita wanatokea nchini Somalia.

Aidha, RC Kunenge amesema hata utaratibu unaotumika kusafirisha watu hao unakiuka Sheria, haki na utu wa binadamu kwa kuwa wengi wao wanafungiwa kwenye kontena zisizokuwa na hewa, na pindi wanapobainika kufariki Dunia maiti zao hutupwa kwenye vichaka.

Kwa upande wake Afisa uhamiaji Mkoa wa Dar Es Salaam Kamishina Msaidizi Edmund Mrosso, amesema kinachofuata baada ya wahamiaji hao kukamatwa watafikishwa Mahakamani kwa kosa la Kuingia nchini kinyume na taratibu.

Aidha, Kamishina Mroso amesema kwa wale wanaowasafirisha au kuwahifadhi wahamihaji hao adhabu inaelekeza kifungo cha miaka 20, faini ya shilingi milioni 20 au vyote kwa pamoja ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zilizotumika.

TFF yabariki usajili wa kimataifa Simba SC
Mirerani, mgodi wenye ulinzi zaidi Tanzania