Wahamiaji haramu 55 raia wa Burundi wamekamatwa na Ofisi ya uhamiaji Mkoa wa Katavi kwa kuingia nchin bila ya kufuata taratibu na kuendelea kufanya kazi za vibarua mashambani, huku wengine wakifanya kazi katika machimbo ya dhahabu na baadhi yao wakiwaingiza watoto wao kusoma katika shule mbalimbali za msingi.

Aidha Kati yao raia hao wa Burundi saba bado wanachunguzwa, 30 watarudishwa Burundi wakiwemo akina mama na watoto, na 15 watafikishwa Mahakamani

Akitoa taarifa ya zoezi linaloendelea la msako, doria na ukaguzi Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Vicent Haule ambaye pia ni afisa uhamiaji wa Mkoa wa Katavi amesema zoezi hilo limefanyika katika maeneo ya Ikola, Ruhafwe na Mpanda

Amesema kumekuwa na wimbi kubwa la uingizaji wa watoto kutoka Burundi kwa ajili ya kuja kupata elimu bure ambapo katika msako unaondelea wamekamata wanafunzi katika shule mbalimbali za msingi

Aidha Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Vicent ameonya juu ya tabia ya kukaribisha raia wa kigeni kwa ajili ya vibarua mbalimbali kama kutunza mifugo na mashamba

Serikali yaindoa tozo 42 kwa wakulima wa Kahawa
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 30, 2022