Boniface Gideon – Tanga

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdarahman ameelezea kuridhishwa kwake na hatua ya Wahifadhi kuhitaji kuwatumia wanasiasa hususani wale wa kutoka Chama tawala katika kuitangaza Sekta ya utalii na hivyo kuwezesha kuleta tija zaidi.

Rajabu ameyasema hayo hii leo ikiwa ni muda mfupi baada ya kukutana na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere Ephraim Mwangomo ambaye alimzawadia Kitabu maalum cha kutunzia Kumbukumbu kama Ishara ya kuimarisha ushirikiano.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdarahman.

Amesema, atawajibika kutumia nafasi yake kupitia majukwaa ya Siasa kuhamasisha Wananchi kutembelea hifadhi zilizopo kwenye maeneo yanayowazunguka kwa vile Utalii siyo kwa ajili ya wageni kutoka nje pekee.

Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, Ephraim Mwangomo.

Kwa upande wake, Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, Ephraim Mwangomo amesema, wahifadhi wamejipanga kushirikiana na viongozi mbalimbali hasa wanasiasa wanaoishi maeneo yenye vivutio vya utalii ili kusaidia kufikisha ujumbe juu ya suala la uhifadhi.

Aidha, Kamishina Mwangomo amesema kuwa ushirikiano huo pia utasaidia kutangaza utalii akisisitiza kusema kwamba iwapo watu wote watazungumza lugha moja itawezesha kukuza sekta hiyo ya utalii hapa nchini.

Adebayor aipeleka Simba SC Morocco
Siri nzito kuondoka kwa Lomalisa Young Africans