Mkuu wa Polisi Wilaya Kibiti, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, John Mwakalukwa aliongoza mazoezi ya ukakamavu katika siku ya Kumbukizi ya Mwl. Julius Nyerere aliyefariki Oktoba 14, 1999 huku akihimiza jamii kufanya mazoezi, ili kuepuka magonjwa nyemelezi.
Akiwa katika eneo hilo, Mwakalukwa aliwataka Wananchi kuendeleza mshikamano wao na Jeshi la Polisi na kuendelea kuwa wazalendo ikiwa ni pamoja na kupenda mazoezi kwa ajili ya afya ya mwili.
Aidha, katika hatua nyingine Mwakalukwa amewaeleza Wananchi umuhimu wa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ya kupiga vita dhidi ya Dawa ya kulevya na umuhimu wa zoezi la usalimishaji wa silaha kwa hiari ambalo linaendelea hadi Oktoba 3, 2023.
Mazoezi hayo yalianzia katika Uwanja wa Samora – Kibiti hadi Kibiti boys na hatimaye kuhitimishwa katika stendi ya mabasi Kibiti na yalihudhuriwa na Askari wa Jeshi la Polisi, Magereza, Jeshi la Wananchi – JWTZ, wananchi na wadau mbalimbali wa michezo Wilaya Kibiti.