Msemaji wa Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO, Christian Lindmeier amesema zaidi ya wahudumu wa afya 160 wamekufa wakati wakitimiza wajibu wao huko Gaza, huku Israel ikidaiwa kupuuzia miito ya usitishwaji mapigano.

Lindmeier ameyasema hayo na kutoa pia wito wa kusitishwa vikwazo kwa misaada ya vifaa vya matibabu, akisema baadhi ya madaktari wamekuwa wakiwafanyia watu upasuaji, ikiwa ni pamoja na kukatwa viungo bila kutumia ganzi.

Aidha, Wizara ya Afya inayodhibitiwa na kundi la Hamas huko Gaza imesema hadi sasa Wapalestinia 10,328 wameuawa ambapo 4,237 kati ya hao wakiwa ni watoto.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi la Kipalestina – UNRWA, limesema asilimia 70 ya watu wameyahama makazi yao huko Gaza huku mzozo kati ya Israel na Hamas ukitimiza mwezi mmoja na ikidaiwa pia Waisrael 1,400 waliuawa na wengine zaidi ya 200 wakitekwa.

Elimu ya ndoa chanzo ukatili, unyanyasaji katika familia
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 8, 2023