Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba iliyopo Mkoani Mtwara, ameyakiwa kuwachukulia hatua watendaji Kata na Vijiji ambao wanaohujumu ugawaji wa pembejeo za Kilimo.
Agizo hilo, limetolewa leo Agosti 13, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa huku Watendaji hao wakitajwa kuwa ni pamoja na Maafisa Kilimo wanaoiba na kuhujumu ugawaaji wa pembejeo za ruzuku, ambazo zimetolewa na Serikali kwa wakulima wa korosho.
Amesema, “suala la mkulima lichukuliwe kwa umakini, ni suala ambalo Raisi aliweka mpaka ruzuku ya Bilioni 50 ili pembejeo zitoshe na ni muhimu zikatosha, ugawaji wa pembejeo katika Wilaya ya Tandahimba imekuwa biashara ya wachache walioko madarakani hii haikubaliki.”
Agizo la Waziri Mkuu, limetolewa baada ya baadhi ya Wakulima kuwalalamikia Watendaji na Viongozi wa ngazi ya Kata na Vijiji wakiwemo Maafisa Kilimo kuwahujumu Wakulima kupata pembejeo, huku wengine wakinyimwa licha ya kuwa wamejisajili.